MWONGOZO KUHUSU BIASHARA NA HAKI ZA BINADAMU

Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu liliidhinisha mwongozo mpya kuhusu uhusiano kati ya biashara na haki za binadamu mnamo Mwaka 2011. Mwongozo ambao kwa mara ya kwanza uliweka misingiya kimataifa ya kukabiliana na athari mbaya zinazotokana na shughuli za biashara kwenye haki za binadamu.

Mwongozo wa biashara na haki za binadamu umetoa wajibu kwa serikali, mashirika ya kimataifa na makampuni mengine ya biashara kulinda na kuheshimu haki za Binadamu.Mwongozo huu unahusisha mataifa na makampuni yote ya biashara, ya kimataifa na mengine bila kujali ukubwa wao.

 

Misingi iliyoainishwa kwenye mwongozo inapaswa kutekelezwa pasipo ubaguzi wa aina yoyote,ukizingatia hasa haki na mahitaji ya binadamu. Pia changamoto zinazowakabili watu kutoka makundi mbalimbali yakijamii. Pamoja na mambo mengine, Mwongozo huu ni mawazo yenye mantiki na yakueleweka, hivyo unapaswa kusomwa na mtu mmoja mmoja na kwa pamoja ili kuweza kufanikisha matokeo chanya na yenye tija kwa watu ,jamii na makampuni ili kuchangia utandawazi endelevu na maisha bora kwa jamii .

Attachments:
FileFile size
Download this file (MWONGOZO-KUHUSU-BIASHARA-NA-HAKI-ZA-BINADAMU-1.pdf)MWONGOZO KUHUSU BIASHARA NA HAKI ZA BINADAMU625 kB